0
KLABU ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.

Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.

Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa
nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa
zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.Suso akafunga bao lake la kwanza tangu
ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la
kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure akacheza rafu ndani ya boksi na Patrick Bamford akaenda kusawazisha dakika za lala salama na katika penalty Liverpool ikashinda
14-13 baada ya Albert Adomah kupoteza
mkwaju wa Boro.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,
Manquillo, Toure, Sakho, Enrique, Rossiter/ Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana, Markovic na Lambert/Balotelli dk74.

Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala, Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter, Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76.

Chapisha Maoni

 
Top