ajili ya kupambana na magonjwa
mbalimbali, wakati mwingine kinga hizi
hushindwa kufanya kazi kutokana na
magonjwa ambayo ni hatari sana hivyo
kuitaji tiba au msaada utakaokuwezesha
kuishi na ugonjwa huo.
Yafuatayo ni magonjwa kumi hatari
usiyopaswa kupuuza katika maisha.
10. MALENGELENGE ni ugonjwa hatari
sana ambao usababishwa na aina mbili
za virusi(HSV-1 na HSV-2) na uambatana
na dalili kama kutapika, homa kali,
vipele au vidonda sehemu za siri na
mdomoni. Ugonjwa huu usipotibiwa
mapema husababisha virusi hawa
kuharibu mishipa ya damu na
kusabababisha kifo.
9.MAFUA MAKALI, Ugonjwa huu pia
usabishwa na virusi vya mafua viitwavyo
influenza A, B na C na usipotibiwa
mapema huaribu mfumo wa upumuaji
na kusababisha kifo.
8. EBOLA, ni ugonjwa hatari sana
uliogundulika mwaka 1976 na
usababisha vifo vingi kutokana na
kuvuja damu ndani na nje ya mwili,
kutapika na mfumo wa hewa kushindwa
kufanya kazi.
7. KIPINDUPINDU, ni ugonjwa wa mlipuko
ambao no hatari sana kwa kupoteza
maisha ya watu wengi kutokana na
upungufu wa maji mwili
unaosababishwa na kuharisha, kutapika
na kukaza kwa misuli.
6. MALARIA ugonjwa huu ni hatari sana
kwani huathiri mzunguko wa damu, ini
na mfumo wa fahamu kwa kasi zaidi
kutokana na kuongezeka kwa vijidudu
vya ugonjwa huu ambavyo
husababishwa na mbu.
5. KUPOOZA, ugonjwa huu usababishwa
na kupooza kwa mishipa ya fahamu
katika ubongo na uti wa mgongo na
kusababisha ulemavu wa viungo au vifo.
4. KISUKARI, tatizo kubwa la ugonjwa huu
ni vigumu kuugundua mapema na hivyo
uendelee kusababisha madhara mpaka
pale unapogundulika huwa katika hatua
mbaya inayosababisha magonjwa ya
moyo, figo, upofu na hata kukatwa
miguu.
3. PUMU ugonjwa huu ni hatari na
humfanya mtu kuwa na aleji ya vitu
vingi na uharibu mfumo wa upumuaji
kutokana na kuvimba na kuziba kwa nja
ya hewa, kukooa, maumivu makali ya
kifua na kushindwa kupumua.
2. MAGONJWA YA MOYO, magonjwa ya
moyo usababisha vifo vingi pale moyo
na mishipa ya damu iaposhindwa
kupeleka damu na hewa ya kutosha
kwenye ubongo na sehemu mbalimbali
za mwili
1. UKIMWI ugonjwa huu ni hatari sana
kwani hauna tiba na usababishwa na
virusi vya ukimwi kutokana na
kushirikiana damu, vitu vyenye ncha
kali, kufanya mapenzi bila kinga na
mama kumwambukiza mtoto aliyeko
tumboni na anayenyonya.
Chapisha Maoni