0
Msikiti wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pili leo. Msikiti huo uliungua kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 13, 2014 k atika ghorofa yake ya juu na
kuteketeza eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa ukarabati.

Leo hii moto huo inasemekana ulianza majira ya saa sita na nusu mchana katika moja ya chumba
ambacho wanafunzi wa kidato cha nne wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtihani wao
wa taifa utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya
Kinondoni Camilius Wambura amethibitisha jambo hilo na kusema kuwa hadi wanafika eneo la
tukio chanzo bado hakijafahamika, na
kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni cha wasichana ambamo magodoro manne yameungua.

“Katika janga la moto uliounguza
madarasa mwezi uliopita Jeshi la Polisi iliunda timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele
na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutaja majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema kwamba “ Sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati
tukivuta muda wa sala ya Ijumaa ndipo tukasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki
hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui." Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima
moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida.


Chapisha Maoni

 
Top