MSHAMBULIAJI Diego Costa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya England.
Mpachika mabao huyo wa Chelsea amefunga mabao manne katika mechi tatu za mwanzo wake
wa kuhamia LIgi Kuu ya England akiwa na Chelsea.
Aidha, baada ya mwanzo mzuri akiwa na
Swansea, Garry Monk ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi huo baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi zake zote tatu, ikiwemo dhidi ya Manchester United Uwanja wa Old
Trafford.
Chapisha Maoni