0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka sita jela, Melkiad Kabunduguru (28) baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu na kukutwa na noti bandia.

Kabunduguru ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom) atatumikia kifungo hicho baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi
uliotolewa dhidi yake.

Katika shtaka la kwanza la Kabunduguru
atatumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu huku shtaka la pili la kukutwa na noti
50 za bandia za Sh5000 mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Juma Hassani alisema mshtakiwa atatumikia vifungo hivyo kwa pamoja baada ya Mahakama kuridhishwa na
ushahidi uliotolewa mahakamani.
Akitoa hukumu hiyo juzi, Hakimu Juma Hassani alidai kuwa mshtakiwa huyo atatumikia kifungo
hicho ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za wizi.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha mashtaka, Felista Mosha uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa
mshtakiwa ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za udanganyifu.

“Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama hii tukufu kutoa adhabu kali dhidi ya mtuhumiwa huyu kutokana na kushamiri kwa vitendo vya
udanganyifu na kujihusisha na matumizi ya noti bandia wakati akijua kuwa ni kosa la kisheria,” alidai Mosha .

Baada ya Hakimu Hassani kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, alimuhukumu Mwiganyi kifungo cha miaka sita jela.

Awali, Wakili wa Serikali, Felista Mosha alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 29, mwaka huu katika Barabara la Ally
Hassan Mwinyi katika mashine ya kutolea fedha (ATM) ya NMB iliyopo Chuo cha Biashara (CBE)
na kujipatia Sh100,000 kutoka kwa Expedith Mtisi kwa madai kuwa angemrejeshea lakini hakufanya
hivyo.
Katika shtaka la pili, mshtakiwa alikutwa na noti bandia 50 za Sh5000.

Chapisha Maoni

 
Top