0
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa
serikali yake imejitolea kumaliza vita nchini nchini
humo. Akiongea kwenye mkutano mkuu wa baraza la umoja wa mataifa mjini New York Kiir ameitaka jamii ya kimataifa kuwashinikiza waasi kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita.

Vita vya kisiasa nchini Sudan Kusini kati ya rais Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu mamalioni ya wengine kuhama
makwao.
Mzozo ulianza mwezi Disemba mwaka uliopita na makubaliano ya kumaliza vita yameshindwa.

Chapisha Maoni

 
Top