WANAJANGWANI, Dar Young
Africans wameitandika 2-1
Tanzania Prisons katika mechi
ya raundi ya pili ya ligi kuu
soka Tanzania bara iliyomalizika
jioni hii uwanja wa Taifa, Dar es
salaam.
Mabao ya Yanga chini ya kocha
Mbrazil yamefungwa na Andrey
Coutinho katika dakika ya 34 na
la pili likatiwa kambani na
Saimon Msuva katika dakika ya
69.
Prisons walijipatia goli la
kufutia machozi katika dakika
ya 67 kupitia kwa Ibrahim Isaka
Hassan.
UCHAMBUZI WA MECHI
Coutinho alifunga goli hilo kwa
mpira wa adhabu ndogo
takribani mita 24. Haruna
Niyonzima aliwadanganya
mabeki wa Prisons kama
anataka kupiga mpira, lakini
akamuachia Coutinho aliyepiga
shuti, mpira ukadunda karibu
na goli, kipa Mohamed Yusuph
akaugusa wakati anajaribu
kuokoa, lakini ukazama ndama
ya nyavu.
Dakika ya 38 Beki wa Prisons,
Jacob Mwalobo aliyekuwa na
kadi ya kwanza ya njano
alioneshwa ya pili na
kuzawadiwa nyekundu na
mwamuzi Andrew Shamba
kufuatia kumfanyia madhambi
Mrisho Ngassa.
Nidhamu mbovu ya ulinzi kwa
mabeki wa Prisons ilisababisha
wakafunwga goli hilo. Wakati
wameweka ukuta waliacha
uwazi na nyuma yao alisimama
Jaja. Coutinho alipiga mpira
ukapita katika eneo hilo na
kutikisa nyavu.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza,
Yanga walitawala zaidi mpira
hususani safu ya kiungo.
Mbuyu Twite akicheza nafasi ya
kiungo wa ulinzi alishirikiana
vizuri na Haruna Niyonzima
aliyecheza mbele yake.
Mrisha Ngassa aliyeshambulia
kutoka kushoto alikuwa
anabadilika na kucheza winga
ya kulia na wakati fulani kuingia
katikati. Hassan Dilunga
aliyeanza winga ya kulia
aligongeana vizuri na Niyonzima
na mara kadhaa alimuacha beki
wake wa kulia Juma Abdul
apande juu kuongeza kasi ya
mashambulizi.
Coutinho alicheza vizuri nafasi
ya kiungo mshambuliaji, ingawa
kuna wakati alikuwa anapiga
pasi mkaa. Jaja kama kawaida
yake hakuonekana sana, kuna
baadhi ya mipira alipata na
kujaribu kupiga kichwa, lakini
hakufanikiwa kufunga goli.
Edward Charles aliyechukua
nafasi ya Oscar Joshua
aliyeumia mechi iliyopita
hakuwa na presha kubwa kwa
upande wake, hivyo alipanda
zaidi kuongeza mashambulizi
kutoka winga ya kulia.
Hata Juma Abdul naye alipanda
zaidi upande wa kulia kuongeza
kasi ya mashambulizi.
Prisons walicheza vizuri, mara
kadhaa walipiga pasi fupifupi,
lakini walikosa kasi ya kwenda
mbele. Walijikuta wakikaa zaidi
katika eneo lao na kuwapa
nafasi Yanga kucheza zaidi safu
nyuma kwasababu walikuwa
wachache. Ngassa alishindwa
kufurahia mechi hiyo
kwasababu Prisons hawakutaka
kutoka katika eneo la pili.
Kipindi cha pili Yanga walianza
kwa kasi kama kawaida na
kulikalia vilivyo dimba la kati.
Dakika ya 55 Dilunga alikwenda
benchi na nafasi yake
kuchukuliwa na Hamis Thabit.
Dakika ya 57, Marcio Maximo
alimtoa Coutinho na nafasi yake
kuchukuliwa na Saimon Msuva.
Kuingia kwa Msuva kuliongeza
kasi zaidi ya Yanga. Dakika ya
61 alitengenezewa pasi nzuri na
Niyonzima na kuachia shuti kali
ambalo halikulenga lango.
Licha ya kuwa pungufu, Prisons
walijitahidi kutengeneza nafasi,
lakini walikosa mshambuliaji wa
kati. Julius Kwanga alipata
nafasi kadhaa, lakini mashuti
yake hayakulenga lango.
Dakika ya 67, Ibrahim Isaka
Hassan alifunga goli safi la
kichwa akiunganisha krosi
iliyochongwa kutoka winga ya
kulia na kuisawazishia Prisons.
Ibrahim aliruka juu, Yondani na
Cannavaro walimuacha huru
kabisa na kipa Dida akajaribu
kuokoa mpira huo , lakini
hakuwa na la kufanya.
Kuingia kwa goli hilo,
kuliwaamusha Prisons na
kuanza kupanda juu, lakini
nidhamu ya ulinzi haikuwa
nzuri.
Dakika ya 69 Saimon Msuva
alifunga goli la pili kwa kichwa
akimalizia krosi ya Ngassa
iliyochongwa kutoka winga ya
kulia.
Ngassa kama kawaida aliburuza
mpira na kuingiza ndani, mabeki
wa Prisons, Jumanne Elifadhili
na Lugano Mwangama
walishindwa kumzuia Msuva.
Licha ya kufunga, Msuva
aliongeza kasi ya Yanga tofauti
na mwanzo na hii ilidhihirisha
kuwa Maximo hakukosea
kufanya mabadiliko hayo.
Dakika ya 81 Ngassa alipata
nafasi ya wazi baada ya
Mwangama kufanya makosa,
lakini alipiga shuti lililotoka
sentimita chache kutoka
langoni.
Licha ya kuwa pungufu, dakika
za lala salama, Prisons
walishambulia lango la Yanga,
lakini walishindwa kuwa na
mipango ya kupata goli.
Mabeki wa Yanga walilazimika
kupigana kufa na kupona
kuokoa jahazi na mpaka dakika
90 zinamalizika, Yanga
walikuwa mbele kwa 2-1
Kwa ujumla kipindi cha pili,
Prisons ilikuja juu na kupiga
pasi nzuri. Walionekana kuwa
na kasi na kuipandisha timu
juu.
Kikubwa walikosa nidhamu ya
mchezo, baada ya kusawazisha
goli walikubali kupanda zaidi
wakati wako pungufu. Ngassa
alikimbizana na beki asiyekuwa
na kasi na wakafungwa aina ya
goli lilelile waliloifunga Yanga.
Prisons si timu ya kuichukulia
poa. Ina upinzani wa hali ya juu
na timu nyingine zijipange
sana.
Chapisha Maoni