0
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesisitiza kuwa hahitaji muda wa mapumziko katika hatua hizo za mwanzo wa
msimu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alipatwa na tatizo la majeruhi mwishoni mwa msimu wa 2013-2014 na wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil.
Hata hivyo, Ronaldo amesisitiza kuwa kwasasa yuko fiti na anataka kuendeleza makali yake aliyokuwa nayo kwa mabingwa hao wa Ulaya baada ya kufuinga mabao ya kutosha katika wiki
chache zilizopita.

Ronaldo alikaririwa akidai kuwa kwasasa wako mwanzoni mwa msimu na anataka kucheza ili kujijengea hali ya kujiamini na wakati utakapofika
wakati muafaka ukifika atapumzika ili aweze kuwapa wenzake nafasi lakini huu sio wakati muafaka.

Mpaka sasa Ronaldo ameshafunga mabao tisa katika mechi nne za ligi alizocheza msimu huu.

Chapisha Maoni

 
Top