Uingereza imeondoa tahadhari iliyokuwea imetoa kwa raia wake dhidi ya Kusafiri Kenya. Tahadhari hiyo kwa ukubwa likuwa inalenga maeneo ya mitaa ya mabanda, na baadhi ya
maeneo ya Pwani ambako ilihofiwa kuwa raia wa kigeni wanalengwa kwa mashambulio ya kigaidi. Hatua hiyo ya kuondolewa tahadhari kwa raia wa
Uingereza kusafiri Kenya, inaanza kutekelezwa mara moja.
Tahadhari hiyo ilikuwa imewekwa baada ya machafuko yaliyotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu yapata miaka saba iliyopita.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza
imewasiliana na wizara ya ndani ya nchi hiyo kwamba hali ya hatari imeshuka kwa kiasi kikubwa.
Wizara hizo zimesema kuwa tahadhari kama hizo hutolewa kuambatana na sera za nchi hiyo za kuwatolea usalama raia wake kote duniani licha ya
taifa linalozungumziwa. Serikali ya Kenya ilikuwa imelalamika kuwa
tahadhari kama hizi zinazotolewa na mataifa ya Magharibi hazina msingi na zinaathiri uchumi wa nchi hiyo.
Chapisha Maoni