Takriban watu 18 wameuawa na watu
wanaoshutumiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram mjini Shaffa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Shuhuda wa tukio hilo amesema mashambulizi hayo yalifanyika siku ya jumatano jioni na kuendelea mpaka alhamisi asubuhi. Wanamgambo wa kiislamu wamesema wameharibu
makanisa kadhaa na makazi mjini humo, na kushambulia kijiji. Mji wa Shaffa uko kwenye jimbo la Borno,jimbo
ambalo limeathiriwa na mashambulizi ya wanamgambo.
Chapisha Maoni