kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa
wanasafiria kuacha njia na kupinduka
katika kijiji cha Michenga, wilaya ya
Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema gari hiyo aina ya Toyota Rava4 yenye namba za usaji T574CWC.Iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalaganya(27) iliacha njia na kupinduka katika barabara ya Ruangwa-
Nanganga, ilitokea jana saa 11.30 jioni. Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua
(51) mkazi wa Tabata Dar-eS-salaam na Elizabeth Chipoleka(53),mkazi wa Yombo, Dar es salaam.
Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), ambapo wote ni wakaazi wa Tabata, Dar es salaam. Dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni na upelelezi unaendelea kujua
chanzo hasa cha ajali hio.
Chapisha Maoni