TIMU ya taifa ya Algeria imefuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Algiers usiku wa jana.
Ushindi huo, unaifanya Algeria ifikishe pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne, wakati Malawi inabaki na pointi zake tatu.
Mali, licha ya kufungwa 3-2 na Ethiopia katika mchezo mwingine wa Kundi B jana, bado wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi sita, wakati Ethiopia ni ya tatu kwa pointi zao tatu pia.Mabao ya Algeria jana yalifungwa na Yacine Brahimi, Riyad Mahrez na Islam Slimani. Katika mchezo wa Kundi G, Tunisia ilipata ushindi mwembamba wa nyumbani 1-0 dhidi ya Senegal Uwanja wa Monastir mjini Tunis, bao pekee la Ferjani Sassi dakika ya 94,
wakati Afrika Kusini imetoka sare ya 0-0 na Kongo Brazaville mchezo wa Kundi A na Burkina Faso imetoka 1-1 na Gabon.
Chapisha Maoni