mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la
kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka
kwa Mwanamme na kumtambua
kama mwanamke licha ya amri
iliyotolewa katika gazeti rasmi la
serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho
kutoka kwa ‘Andrew Mbugua’ na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la
‘Audrey Mbugua’ bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey
kwenye cheti hicho haiongezi
thamani yoyote kwa matokeo yake
wala alama alizopata Audrey na
kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
‘Audrey ni mwanadamu ambaye
anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia
aliyozaliwa nayo,” alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi
inaamrisha watu kuwaheshimu
wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi
ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi
kuwa sawa anapaswa kukubalika
kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa
haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia
mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea
matibabu.
Chapisha Maoni