Wamesema Dukalheen Bai alikufa baada ya kufungwa, kupigwa na kuteswa kwa saa kadha na shemeji yake, Nakul Patel na ndugu wengine wa familia.
Bwana Patel anaaminika kumshutumu Bi Dukalheen Bai kumsababishia ugonjwa mtoto wake wa kiume kutokana na vitendo vya kishirikina.
Vitendo vya kuwasaka wachawi wakiwalenga wanawake ni vitendo vya kawaida katika sehemu mbalimbali za India na wale wanaotuhumiwa
wanauawa kila mwaka.
Tukio la hivi karibuni limetokea katika wilaya ya Bemetara katika jimbo la kati la Chhattisgarh.
Bwana Patel ni miongoni mwa watu 10,wakiwemo wanawake watano waliokamatwa kufuatia mauaji
hayo. Bwana Patel bado hajatoa kauli yoyote hadharani kuhusiana na kitendo hicho alichofanya.
"Mama yangu alipigwa vibaya. Aliendelea kupiga yowe lakini kijiji kizima kiliangalia tu kilichokuwa
kikifanyika. Nilipinga kitendo hicho, lakini sikuweza kumsaidia mama yangu," Ashok Patel mtoto wa
kiume wa Dukalheen Bai 'ameiambia Idhaa ya Kihindi ya BBC.
Kuwapakazia wanawake uchawi ni mambo yanayotokea hasa katika jamii za kikabila nchini India.
Wataalam wanasema imani za kishirikina zimechochea mashambulio haya, lakini matukio haya yanatumika kama kivuli tu kwa watu, hususan wajane wanapotakiwa kunyang'anywa
ardhi na mali zao.
Mapema mwezi huu, mwanariadha Debjani Bora, mtupa mkuki ambaye ameshinda medali kadhaa
za dhahabu, aliiambia BBC namna alivyofungwa na Kupigwa vibaya baada ya kuitwa mchawi katika kijiji chake kaskazini-mashariki mwa jimbo la
Assam.
Chapisha Maoni