ameanza ziara ya kuzitembelea nchi tatu
zilizoathirika zaidi na mlipuko wa Ebola, akikosoa msaada wa kimataifa katika kukabiliana na ugonjwa huu.
Samantha Power ametua Guinea na atatembelea Sierra Leone na Liberia.
Ameliambia shirika la Utangazaji la Marekani, NBC kuwa baadhi ya mataifa ambayo yaliahidi msaada "bado hayajawajibika" katika kutoa msaada na
madaktari.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani za hivi karibuni, zaidi ya watu 10,000 wameambukizwa virusi vya Ebola, huku watu 4,922 wakipoteza maisha.
Wagonjwa hawa ni kutoka nchi za Sierra Leone, Liberia na Guinea, isipokuwa 27 kati yao.
Bi Power ameiambia NBC wakati akipanda ndege yake yenye maandishi: "Mwitikio wa kimataifa
kuhusu Ebola unatakiwa kuchukuliwa kwa namna tofauti kabisa kuliko ilivyo sasa hivi."
Amesema: "Mna nchi katika Umoja wa Mataifa ambako nafanyakazi kila siku watu ambao wanatia saini maazimio na kusifia kazi nzuri ya Marekani
na Uingereza na nyinginezo, lakini wenyewe hawajachukua hatua zozote za kuwajibika kwa kuwatuma madaktari, kutuma vitanda, na kutoa kiasi cha fedha kinachofaa."
Samantha Power amekuwa mkosoaji kuhusu mwitikio wa kimataifa katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Atatembelea vituo vya kitaifa vya kuratibu shughuli za kukabiliana na Ebola na kukutana na wafanyakazi wa Marekani na Umoja wa Mataifa,
ingawaje haikuwekwa wazi kama atakutana na watu walionusurika kifo baada ya kuugua Ebola.
Marekani imeahidi wanajeshi 4,000 kujenga hospitali na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya, Afrika Magharibi, ambapo askari 600 tayari
wamewasili huko.
Chapisha Maoni