0
Msanii wa Bongo fleva Queen Darleen ambae pia ni Jaji wa mashindano ya kucheza Dance 100% 2014 amefunguka na kuweka wazi kuwa katika
maisha yake hajawahi kutoka kimapenzi na msanii mwenzake wa Bongo Fleva Ali Kiba Queen Darleen amefunguka hayo leo alipokuwa akichat Live kupitia kurasa wa Facebook wa EATV
katika kipengele cha Kikaangoni Live
kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mpaka saa nane mchana.

Queen Darleen amesema hayo leo baada ya watu wengi kuuliza maswali kutaka kujua juu ya mahusiano yake na msanii Ali Kiba ambapo alikana kuwa na mahusiano na mkali huyo wa
Bongo Fleva ambae kwa sasa anatamba na ngoma zake mbili Mwana na Kimasomaso ila Queen Darleen aliweka wazi kuwa anamkubali msanii huyo kisanaa kwani katika wanamuziki
aliowahi kushirikiana nao Ali Kiba ndiye
anaemkubali zaidi.Pia aliongeza kuwa kwa wasanii wa bongo fleva wa hapa nyumbani anamkubali na
kumpenda Ali Kiba kutokana na uwezo wake kimuziki.

UHUSIANO WAKE NA DIAMOND
Mbali na hilo msanii Queen Darleen aliweka wazi uhusiano wake na msanii wa Bongo fleva Diamond Platnum na kusema kuwa ni kaka yake wa damu na wana share baba mmoja,katika
kuelezea namna ambavyo anaweza kusonga mbele katika sanaa japo kufikia kiwango ambacho kaka yake amefikia kimuziki,Queen Darleen alisema ni kazi ngumu kwake kufikia kiwango
hicho ingawa anadai atazidi kukomaa kibishi japo aweze kusonga mbele zaidi.

Lakini mashabiki wengi walimtaka dada huyo wa Diamond Platnum kumshauri kaka yake apunguze michepuko na jibu la Queen Darleen lilikuwa ni
fupi kuwa atafikisha ujumbe huo kwa muhusika.


HARAKAZI ZA MAISHA
Qeen Darleen amesema kuwa katika harakati zake za kusaka maisha alipomaliza shule kidato cha
nne alisomea fani ya nessi ili aje kutoa huduma ya Nurseing kwa jamii ingawa baadae haikuweza kuwa hivyo tena kutokana na kujikita katika
kufanya muziki na kujikuta maisha yake
akiegemea zaidi katika muziki kuliko hata hiyo fani aliyosomea baada ya kumaliza kidato cha nne.

Queen Darleen ambae ni mama wa mtoto mmoja ambae amempa jina la Rooney amesema kuwa
anajivunia kuwa mama ingawa hana mpango wa kuolewa kwa sasa.Ingawa yupo katika mahusiano na mpenzi wake wa zamani ambae anafahamika
kama Moses Clement.

VIGEZO VYA MAKSI KWENYE MASHINDANO YA
DANCE 100%
Queen Darleen ambae ni moja ya jaji kati ya jopo la majaji katika shindano la Dance 100% 2014 ambalo linafikia tamati siku ya Jumamosi
amesema kuwa katika shindano hilo yeye kama jaji pamoja na majaji wenzake wanakuwa
wakiangali vitu vingi katika kutoka maksi kwa kundi husika hivyo hawakurupuki kutoa tu maksi bali kuna vigezo ambavyo wanatafuta na kuviangalia katika kila kundi ndio maana wanatoa
maksi pasipokupendelea kwa kuwa kuna vigezo ambavyo wahusika lazima wawenavyo pindi wanapokuwa
wakicheza jukwaani.

BIFU YA ALI KIBA NA DIAMOND
Mashabiki wa ukurasa wa EATV walitaka kujua ukweli juu ya bifu kali inayoendelea mtaani kati ya mashabiki wa muziki wa Ali Kiba na Diamond
Platnum hivyo walitaka kujua kama watu hao kweli wa bifu au laah,na waliweza kuuliza maswali hayo kwa kuwa Queen Darling amekuwa karibu
sana na Msanii Ali Kiba pia ni dada wa Diamond Platnum hivyo wameamini kuwa huenda atakuwa na ukweli juu ya suala hilo.

Said R Said>>>>>>Vipi kuhusu Diamond na Ali Kiba eti ni kweli hawaelewani kisa? Kama ni kweli kisa nini na wewe unafahamiana nao wote? QueenDarleen Abdul>>>Hapanaaaa bana mbona
maswaiba sanaaaaa wale hivyo hakuna bifu yoyote ile.

Chapisha Maoni

 
Top