Mbovu (Masasi ya zamani) mjini Masasi
wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za
kucheza uchi, kwa staili inayoitwa
Kigodoro kwenye sherehe ya ndoa.
Mkuu wa Polisi wilayani Masasi, Ndagile
Makubi jana alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa watuhumiwa
hao walikamatwa juzi jioni katika eneo la
Masasi mbovu watuhumiwa kutokana na
kucheza wakiwa watupu kunakokiuka
maadili ya Kitanzania.
Alisema walipata taarifa za kuwepo kwa
tukio hilo la kiudhalilishaji kutoka kwa
wasamaria wema waliokuwepo kwenye
sherehe hizo na kwamba Polisi walifika
na kufanikiwa kuwatia mbaroni
watuhumiwa hao waliokutwa wakiwa
wanaendelea kutoa burudani hiyo kwa
mamia ya watu waliojitokeza kwenye
sherehe hizo wakiwamo watoto.
Makubi aliwataja wanaoshikiliwa na
jeshi hilo kuwa ni pamoja na Anna
Yohana (25), Jemima Jordan (22), Aziza
Chukachuka (20) na mtoto wa miaka 17
(jina linahifadhiwa) wote wakiwa ni
wakazi wa mjini Masasi mkoani Mtwara.
Alisema uchunguzi unaendelea na
kwamba watakapobainika kuhusika na
tukio hilo la udhalilishaji hasa kwa jinsia
ya kike watafikishwa mahakamani kwa
taratibu zingine za kisheria.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Tiba
Matwani na Fatuma Hamisi
wamepongeza Polisi wilayani Masasi kwa
kuanza operesheni hiyo na kwamba
vitendo hivyo vinavyofanywa na
wanawake wenzao havistahili kuachiwa
vikiendelea kwa kuwa vinadhalilisha utu
wao.
Aidha, Kamanda Makubi alizungumzia
mikakati iliyowekwa na jeshi hilo mjini
humo, ikiwa ni pamoja na kuendesha
operesheni maalumu kwenye maeneo
yote ya burudani na sherehe mbalimbali
ili kuwabaini watu wote wanaokwenda
kinyume na maadili ya Kitanzania.

Chapisha Maoni