mizigo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar
esalaam kwenda Zambia yameteketea
baada ya treni hiyo kuanguka katika Kijiji
cha Kifulu, mkoani Pwani.
Treni hiyo iliyokuwa na mabehewa 35,
ilikuwa ikisafirisha mbolea aina ya
sulphur. Kichwa cha treni hiyo kiliacha
njia na mabehewa saba kati ya 21
kutumbukia kwenye mtaro.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya
mashuhuda, Faraji Abduli, Seif Juma
Aziza Salimu walisema mabehewa hayo
yalianguka jirani na mashamba ya
wananchi yaliyokuwa yakisafishwa kwa
kuchomwa moto.
Kutokana na moto huo, mabehewa
matatu kati ya saba yaliyoanguka,
yalishika moto uliosambaa kwenye
mabehewa mengine mawili na
kuyateketeza.
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia baadaye
zilidai kuwa kuungua kwa mbolea hiyo
kumesababisha madhara kwa baadhi ya
wakazi wa eneo la jirani kutokana na
moshi kuwaumiza vifua na kusababisha
wakohoe.
Kaimu kamanda wa polisi wa Pwani,
Mrakibu Mwandamizi SSP Athumani
Mwambalaswa alisema:
“Mabehewa 21 yamerudishwa Tazara na
taarifa za tukio hilo zitatolewa na Ofisi ya
Tazara Dar es Salaam.”
Akizungumzia madhara waliyopata
wananchi kutokana na kukohoa
kulikosababishwa na moshi huo wa
kuungua mbolea, Mwambalaswa alisema
wanajitahidi kuwasiliana na wataalamu
wa afya ili wafike eneo la tukio.
“Hili la watu kukohoa, siwezi kuthibitisha
kwa sasa, maana sisi siyo wataalamu wa
afya hadi watakapofika wahusika,”
alisema na kuongeza: “Nimewasikia
wananchi wakilalamika, lakini mambo yote
haya yatazungumzwa na ofisi Tazara na
siyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.”
Chapisha Maoni