Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema
kuwa Bi Julia Pierson (pichani) , Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Rais wa Marekani maarufu kama Secret Service, amejiuzuru nafasi hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wan chi hiyo Bw. Jeh Johnson ametangaza
leo. Katika taarifa yake Bw. Johnson
kasema atamteua Bw. Joseph Clancy
kukaimu wadhifa huo nyeti.
Afisa habari wa Ikulu ya Marekani Bw.
Josh Earnest amesema katika mkutano na wanahabari leo kuwa Rais Barack Obama
alimwita Bi Pierson na kumshukuru kwa
utumishi wake katika Idara hiyo na nchi ya
Marekani, na kwamba Rais huyo aliweka
bayana kwamba iko haja ya kuwa na
uongozi mpya katika Idara hiyo.
Akiongea baada ya uamuzi huo wa kuachia ngazi, Bi. Pierson alisema ulikuwa ni uamuzi mchungu. “Nadhani (uamuzi huo)
kwa maslahi ya Secret Service na umma wa Wamarekani. Congress (Bunge) limepoteza imani name kuongoza Idara hii. Vyombo vya habari navyo vimeweka bayana kuwa hili ndilo wanalotarajia. Ni uchungu
kuacha kazi katika Idara hii ambayo
inaandamwa na kashfa mbalimbali za
uwajibikaji mbovu wa usalama”.
Bi Pierson alikuwa amekalia kuti kavu na
kuwekwa katika hali ngumu kufuatia
matukio kadhaa ya kuhatarisha usalama
(wa Rais), ikiwa ni pamoja na mtu mmoja kuruka uzio wa White House na kuingia ndani akiwa na kisu mkononi mnamo Septemba 19 mwaka huu.
Inaripotiwa kuwa
aliingia humo ndani baada ya kumzidi
nguvu afisa usalama aliyekuwa lindo,
kabla ya kuzidiwa nguvu na afisa mwingine
aliyekuwa amemaliza zamu.
Baada ya tukio hilo, matukio mengine ya
kuhatarisha usalama wa Rais yakaibuka.
Moja likiwa ni kuruhusiwa kwa mtu mmoja aliyewahi kufungwa jela kuingia katika lifti moja na Rais Obama alipokuwa akizuru
Taasisi ya kuzuia magonjwa mwezi
uliopita. Pia kuna tukio la mtu kupiga
risasi Ikulu hiyo ya Marekani ambayo pia
ni makazi rasmi ya Rais wa Marekani.
Jumanne iliyopita Bi Pierson aliwekwa
kitimoto na kamati ya Bunge kuhusu
matukio hayo. Alisema tukio la karibuni
lilikuwa halikubaliki na akakiri udhaifu wa idara katika majukumu yake. “Nakubali kubeba lawama zote”, alisema. “Haitotokea
tena.

Chapisha Maoni