0
Ajali kubwa ya moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika, imetokea na kuteketeza bweni la wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mtakatifu Petro iliyopo eneo la Iwanzari, Tabora pamoja na
vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo.

ITV wameripoti kuhusiana na tukio hilo, ambapo moto huo umezuka ghafla wakati wanafunzi wakiwa katika ibada na hata baada ya taarifa kuwafikia askari wa kikosi cha zimamoto hawakutoa ushirikiano wowote kwa madai kuwa
magari ya kuzima moto ni mabovu kitendo kilichowasikitisha mkuu wa shule hiyo Simon Kyala pamoja na askofu wa kanisa hilo Mhashamu
Elias Chakupewa.

Meya wa Tabora, Gulam Dewji na mratibu mwandamizi mkuu wa kikosi cha zimamoto Tabora, Kondo Mwamed wamesema manispaa ina gari moja na liko katika matengenezo kwa
takribani miezi 2. Thamani ya vitu vilivyoteketea bado haijafahamika
japo mkuu wa shule amekiri kuwa wanafunzi hao wameathiriwa na janga hilo kipindi ambacho wanakaribia kuanza mitihani.

Chapisha Maoni

 
Top