MECHI ya kufuzu kwa Fainali za Euro 2016 baina ya Serbia na Albania ilivunjika baada ya dakika 30 usiku wa jana, kufuatia beki wa Serbia, Stefan Mitrovic kuitupa bendera ya
Albania na kusababisha Uwanja wa Partizan, mjini Belgrade kugeuka sehemu ya mapambano.
UEFA iliwafungia mashabiki wa Albania
kuhudhuria mechi hiyo ya Kundi I mjini
Belgrade, lakini iliruhusu nchi hizo mbili
kumenyana, licha ya uhasama wa muda
mrefu wa kisiasa baina yao. Na wakati bendera ya Albania iliyoambatana
na ramani ya Kosovo na ujumbe wa
'autochthonous', wenye kumaanisha asili- ikipeperushwa juu ya eneo la kuchezea kwa kutumia rimoti, kitendo cha Mitrovic kuirukia na kuitupa kilisababisha balaa, wachezaji kwa
wachezaji na mashabiki kuanza kupigana.
Chapisha Maoni