CHELSEA imeinyamazisha Arsenal baada ya kuichapa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Mabao ya Chelsea inayofundishwa na Mreno,
Jose Mourinho yamefungw ana Edin Hazard kwa penalty dakika ya 27 na Diego Costa dakika ya 78.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo,
Tottenham Hotspur imeilaza 1-0
Southampton, bao pekee la Christian Eriksen dakika ya 40.
Mchezo uliotangulia mchana wa leo,
Manchester United wameshinda 2-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Old Trafford jioni hii. Angel di Maria alitangulia kuifungia Manchester United dakika ya 26 kabla ya mkwaju wa penalti wa Leighton Baines kuokolewa na David de Gea dakika ya 45 baada ya Tony Hibbert kuchezewa rafu na Luke Shaw.
Everton ilisawazisha bao hilo dakika ya 55 kupitia kwa Steven Naismith akimalizia krosi nzuri ya Baines kabla ya Radamel Falcao kuifungia bao la ushindi Manchester United
dakika ya 62.
Chapisha Maoni