MANCHESTER United imepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa mabao 2-1 Everton Uwanja wa Old Trafford jioni hii.
Hali sasa ni shwari kwa kocha Louis Van Gaal baada ya ushindi huo mshambuliaji wake wa mkopo, Radamel Falcao akifunga bao lake la kwanza tangu atue Old Trafford.
Angel di Maria alitangulia kuifungia
Manchester United dakika ya 26 kabla ya mkwaju wa penalti wa Leighton Baines kuokolewa na David de Gea dakika ya 45 baada ya Tony Hibbert kuchezewa rafu na
Luke Shaw.
Everton ilisawazisha bao hilo dakika ya 55 kupitia kwa Steven Naismith akimalizia krosi nzuri ya Baines kabla ya Radamel Falcao kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya 62.
Chapisha Maoni