0
CHELSEA imepata ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Sporting Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Roma ya Italia usiku huu.

Katika mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja Matic dakika ya 34 limemfanya kocha Jose Mourinho aitambie timu ya nchini kwake, Sporting.



Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero alitangulia kuifungia City kwa penalti dakika ya nne kabla ya mkongwe Francesco Totti kuisawazishia
Roma dakika ya 23 katika mchezo wa Kundi E.
Bao pekee la Thomas Mueller dakika ya 22 limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo mwingine wa Kundi E. mchezo mwingine wa kundi hilo usiku Schalke
04 imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Maribor.


Kundi F, PSG imeichapa FC Barcelona mabao 3-2, mabao yake yakitiwa kimiani na David Luiz dakika ya 10, Marco Veratti dakika ya 26 na Blaise Matuidi dakika ya 54, wakati mabao
ya wageni yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 12 na Neymar dakika ya 56.

Mchezo mwingine wa Kundi hilo, APOEL
Nicosia imelazimishwa sare ya 1-1 na Ajax nyumbani bao la wenyeji likifungwa na Manduca dakika ya 31 na la wageni
likifungwa na Lucas Anderson mapema dakika ya 28.


Kundi H, BATE Borisov imeichapa 2-1
Athletic Bilbao nyumbani mabao ya washindi yakifungwa na Denis Polyakov dakika ya 19 na Karnitskiy dakika ya 41, wakati bao la wageni lilifungwa na Aritz Aduriz dakika ya 45.

Shakhtar Donetsk imelazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na FC Porto, mabao ya wenyeji yakifungwa na Alex Teixeira dakika ya 52 na Luiz Adriano dakika ya 85, wakati ya wageni yote yamefungwa na Jackson Martinez dakika
ya 89 kwa penalti na 90.

Chapisha Maoni

 
Top