0
ACT-TANZANIA
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa Watanzania
kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.
Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA
CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

Act-Tanzania tunaeleza kuwa ni chama cha Watanzania wote kisichokuwa na mmiliki wake na tunaunganishwa na misingi kumi ya chama
pamoja na Itikadi yetu ya demokrasia jamii.

Act-Tanzania tunatambua uwezo na mchango wa kisiasa na ujenzi wa demokrasia ya vyama vyingi
nchini uliotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Na kwamba kwa sasa ana kesi na chama chake mahakamani na tunaamini atakapomaliza kesi hiyo mchango wake katika siasa za upinzani za
Tanzania ni muhimu sana.

Act-Tanzania tunaamini kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa mahiri na makini hivyo tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu katika chama mbadala Tanzania.

Na kuhusiana kwamba kuna mkakati wa kuipa nguvu Act-Tanzania ni taarifa za kutunga kwani mikakati yetu ya kuimarisha chama na uenezi
wake ni mkubwa na mipango yetu inayotekelezwa kwa umakini na weledi mkubwa.

Na Act-Tanzania tumejipanga kufanya siasa zitakazoleta mabadiliko nchini na kasi yetu inatokana na juhudi na mshikamano wa viongozi
wa ngazi zote. Aidha tunatumia eneo kubwa la mipango yetu ya
kukieneza chama kwa mfano kwa sasa
tumemaliza ziara ya mikoa 12 na majimbo 68 hivi karibuni iliyokuwa na mafanikio makubwa sana.

Pamoja na mambo mengine tulitoa maelekezo ya maandalizi ya uchaguzi wa vijiji, vitongoji na serikali za mitaa tarehe 14/12/2014, tukitekeleza
azimio la kikao cha Halmashauri kuu
kilichofanyika Singida. Hivyo hakuna mkakati wa kuibeba ACT-Tanzania,
Bali ACT-Tanzania inabebwa na umakini na weledi katika mipango yake.
Kuhusu Bwana Samson Mwigamba na Profesa Kitilia Nkumbo kujiunga na Act-Tanzania hawa ni Watanzania na baada ya kufukuzwa na chama
chao cha zamani Act-Tanzania tuliona mchango wao bado unahitajika katika siasa hapa nchini na kwa kuwa hakukuwa na kizuizi kwa wao kujiunga
na Act-Tanzania basi tuliwapokea na kwa sasa wanatumikia Act-Tanzania kwa moyo wa kizalendo kabisa.

Kuhusiana na hoja ya kwamba kuna mamluki wa upinzani hizo ni siasa nyepesi kwani unapofukuza
wanasiasa mahiri ndani ya chama chochote na wanapokosa fursa ya kufanya siasa pale walipofukuzwa hakuna dhambi ya kushiriki siasa
katika chama kipya cha siasa hapa nchini.

Mwisho tunawashukuru Watanzania wote wanaoendelea kutuunga mkono nchini kote. Pia tunapenda kutoa tamko kwamba kwa mujibu
wa maazimio ya kikao cha Halmashauri kuu kilichokutana mjini Singida tarehe 25-26/7/2014 tunaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa
vijiji,vitongoji na serikali za mitaa na maandalizi yetu yanaendelea vyema kabisa.

Lakini pia tunaheshimu uhuru wa kutoa habari waliotumia gazeti la Mwanahabari lakini tumesikitishwa sana na wao kama chombo huru
kushindwa kutuhoji sisi kama chama baada ya kuwa na habari wanayoiita 

"MKAKATI WA KUKIPA
NGUVU CHAMA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

Imetolewa Leo tarehe 01/10/2014
Na Mohammed Massaga Katibu mawasiliano na Uenezi wa ACT-TANZANIA
Taifa

Chapisha Maoni

 
Top