Mwanamke mmoja katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara, amemfanyia ukatili mume wake kwa kumwagia maji ya moto yaliyokuwa yametengwa
kwa ajili ya kupikia ugali. Kwa mujibu wa jeshi la polisi wilayani hapa, tukio
hilo lilitokea juzi, saa 4:30 usiku, katika mtaa wa Nyamakokoto, mjini Bunda, baada ya kuzuka ugomvi ulitokana na mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) kuchelewa kurudi nyumbani.
Mwanaume huyo amejeruhiwa vibaya mume wake sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyopelekea kulazwa katika Hospitali Teule ya
Wilaya ya Bunda.
Akizungumza na NIPASHE juzi, mwanaume huyo alisema sababu ya mke wake kummwagia maji ya
moto ni kumuuliza sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kwani alirudi saa 4:30 usiku.
Alisema siku hiyo alitoka kazini kwake saa 1:00 usiku na kukuta mke wake ambaye amezaa naye watoto wanne akiwa hajarejea nyumbani huku
watoto hawajetengewa chakula.
Alisema baada ya kukuta hali hiyo aliamua kuchukuwa fedha na kwenda kununua mboga ili aweze kuandaa chakula cha usiku akijua hawezi
kurudi muda huo.
Alisema baada ya kufika saa 4:00 usiku wakati watoto wake wameshabandika maji ya kupikia ugali, aliamua kwenda kwa rafiki wa mke wake ili
kuuliza alipo mkewe, lakini walisema
hawajamuona.
Alisema aliamua kurejea nyumbani na ilipofika saa 4:30 usiku mwanamke huyo alirejea na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa kiasi hicho, alichukuwa sufuria la maji ya moto na kumwagia.
“Tangu nimuowe na kufanikiwa kuzaa naye watoto wanne sijawahi kumpiga licha ya kufanya vituko vya mara kwa mara….sasa aliporejea muda wa
saa 4:30 na mimi kumuuliza ni kwani amechelewa kiasi hicho na akijua ni mke wa mtu, hapo ndipo alipochukuwa maji ya moto yaliyokuwa
yametengwa kwa ajili ya kupikia ugali na
kunimwagia” alisema.
Mganga wa zamu katika hospitali ya Bunda, Dk. Bakari Ibrahimu, alisema majeruhi huyo amejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa kifuani na mikononi na kwamba
anaendelea na matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kuongeza kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
CHANZO: NIPASHE
Chapisha Maoni