0
Shirika moja la hisani limeonya kuwa kiwango cha visa vitano vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kila saa nchini Sierra Leone inamaanisha kuwa
kuna uhaba mkubwa wa vituo vya afya nchini humo.

Save the Children limesema kuwa kuna visa 765 vipya vya Ebola ambavyo vimeripotiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku kukiwa kuna vitanda
327 pekee nchini humo.

Wataalam na wanasiasa wanatarajiwa kukutana mjini London ili kujadili mbinu mpya za kutatua tatizo hilo.
Ni mlipuko hatari wa ugonjwa huo kuwahi kutokea baada ya kuwaua watu 3338 kufikia sasa. Kuna visa 7,178 ambavyo vimethibitishwa huku
mataifa ya Sierra Leone ,Liberia na Guinea yakiathirika vibaya.

Shirika hilo linasema kuwa ugonjwa huo
unasambaa nchini Sierra Leone kwa kasi mno huku visa vipya vinavyoripotiwa vikiongezeka mara mbili kila wiki.

Limesema kuwa hata baada ya maafisa wa afya kukabiliana na mlipuko huo katika eneo moja ,ugonjwa umekuwa ukisambaa katika maeneo
mengine.
Vilevile viwango vya ugonjwa huo havijaripotiwa kama inavyotakikana kwa kuwa watoto wengi wanaendelea kufariki majumbani mwao ama hata
barabarani bila kujulikana.
Mapema mwezi huu ,Uingereza ilisema kuwa itajenga vituo vya afya vyenye vitanda 700 nchini Sierra leone ,lakini vitanda hivyo havitakuwa tayari
baada ya wiki moja na kwamba vyengine
vitachukuwa miezi kadhaa kukamilika.
Save the Children limesema kuwa iwapo jamii ya kimtaifa haitachukua hatua ,raia wengi wataendelea kufariki majumbani mwao mbali na kutishia kuwaambukiza watu wengi wa familia na jamii
nzima kwa jumla.

Chapisha Maoni

 
Top