Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema anayedaiwa kutoroshwa na mchungaji huyo.
**********
Mchungaji anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba
amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchungaji huyo alifika nyumbani kwa Jonas Mrema, mume wa Janet, maeneo ya Tegeta-Nyaishozi jijini Dar na
kuishi kama mtumishi wa Mungu lakini polepole alianza mazoea tata na Janet.
“Mume alianza kuhisi mabadiliko ya mkewe kwa mtumishi huyo, lakini nadhani aliona ni mawazo
yake tu. Ndipo siku ya siku akashangaa mkewe na mchungaji huyo wameondoka nyumbani hapo.
“Kwa sasa tangu tukio hilo litokee ni miezi kama mitatu. Mume alihangaika sana kumtafuta mkewe hadi jana (Jumatatu iliyopita) ndipo akampata
wakiwa na mchungaji huyo kwenye nyumba moja ambako walikuwa wakiishi pamoja,” kilisema chanzo chetu.
Iliidaiwa kwamba, mchungaji huyo alipopekuliwa alikutwa na paspoti ya nchini Burundi wakati yeye
ni Mkongo wa Uvira na alionekana kuishi nchini kinyume na sheria hivyo alifunguliwa jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hili, Tegeta lenye Kumbukumbu Na. WH/ RB/7040/2014- KUISHI NCHINI BILA KIBALI.
Juzi, Amani liliwasiliana na Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari chama hicho kimemsimamisha uanachana Janet kwa
kitendo chake hicho cha kumtoroka mumewe wa ndoa.
“Ni kweli na Chama cha Waimba Injili Tanzania kimemsimamisha uanachama Janet. Hatuna mzaha katika maadili,” alisema Stela. Amani lilimpigia simu mume wa Janet, Jonas Mrema ambapo katika mazungumzo baada ya salamu alipewa pole kwa matatizo ya mkewe,
alisema asante kisha alipoulizwa kuhusu hali ilivyo aliomba apige simu yeye baadaye kwa vile alikuwa kikaoni.
Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita bila kupiga, Amani lilimpigia tena simu ambapo iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
Chanzo: Gazeti la Amani
Chapisha Maoni