HISPANIA imechapwa mabao 2-1 na Slovakia katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2016 usiku wa jana ugenini, huku mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ‘akitiwa mfukoni’.
Shukrani kwake, nyota wa Slovakia, Miroslav Stoch aliyefunga bao la ushindi dakika ya 87 kuipa timu yake pointi tatu muhimu. Kipa wa Real Madrid, Iker Casillas alifanya makosa yaliyoipa Slovakia bao la kuongoza
lililofungwa na Juraj Kucka dakika ya 17,
kabla ya Paco Alcacer aliyetokea benchi
kuisawazishia Hispania dakika ya 83.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Hispania katika mechi za kufuzu baada ya miaka nane- katika mchezo ambao Diego Costa hakufurukuta na alilimwa kadi ya njano dakika ya 90.
Kikosi cha Slovakia kilikuwa: Kozacik,
Pekarik, Skrtel, Durica, Hubocan, Mak/Stoch dk61, Pecovsky, Gyomber, Kucka/Kiss dk83, Weiss/Duris dk54 na Hamsik.
Hispania: Casillas, Juanfran/Cazorla dk81, Pique, Albiol/Pedro dk58, Jordi Alba, David Silva/Alcacer dk71, Busquets, Fabregas,
Koke, Iniesta na Diego Costa.
Chapisha Maoni