Serikali ya Tanzania imepeleka wataalam wa afya nchini Sierra Leone na Liberia kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imesema wataalam hao watahudumu katika nchi hizo kwa kipindi cha miezi mitatu.
Hatua hii imefikiwa kama mbinu mojawapo ya kuuzuia ugonjwa huo kusambaa zaidi duniani. Akizungumza na BBC mjini Dar es Salaam
msemaji wa wizara hiyo Nsachris Mwamwaja amesema serikali imelichukulia jambo hilo kwa uzito mkubwa wenye msukumo wa kibinadamu zaidi na ni kuitikia wito wa dunia kwamba Ebola sasa ni janga kubwa katika eneo la Afrika
Magharibi na baadhi ya maeneo mengine.
Wataalamu hao ni Dr Theophili Malibicha, Justin Maeda, Godbless Lucas, Herilinda Temba na
Saasita Ramadhan.
Baadhi ya wataalam hao waliojitolea kwenda kupambana na Ebola wamesema wanajiamini kwa uamuzi waliochukua na hawakulazimishwa na mtu.
Chapisha Maoni