
Malta ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Michael Mifsud kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Alessandro Florenzi. Mchezo mwingine wa Kundi hilo, Croatia imeilaza Azerbaijan 6-0 mabao yake yakifungwa na Andrej Kramaric, Ivan Parisic
mawili, Marcelo Brozovic na Luka Modric wakati lingine Sadygov alijifunga.
Norway imeifunga Bulgaria 2-1, mabao yake yakitiwa nyavuni na Elyounoussi dakika ya 13 na Haavard Nielsen dakika ya 72, wakati la wapinzani wao limefungwa na Nikolay Bodurov dakika ya 43.
Chapisha Maoni