0
Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa
wanakutana katika maeneo mbalimbali,
wapo wanaokutana vyuoni,shuleni,
kwenye nyumba za ibada, sokoni,
kwenye daladala, kuunganishwa na mtu
mwingine, au baada ya kusikia sauti
kwenye simu, redioni, hotelini na sasa
wengine kupitia mitandao ya kijamii
kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao
unapoanzisha uhusiano na mtu
usiyemfahamu inawezekana ameona
picha yako tu nakukuambia kuwa
anakupenda na wewe ukiona picha yake
ukaridhika naye mkaamua kuanzisha
uhusino ni vyema kuonana kabisa ili
kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka
kuanzisha kwani unahitaji kumfahamu
zaidi na ndipo utakapoweza kufanya
maamuzi ya kukubali au kukataa.

Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida
lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana
mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka
na kutaka kuoana haraka haraka na yule
ambaye mna chat tu kwenye mitandao
unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa
maamuzi yako ni vyema kufahamiana
zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na
maamuzi yako....Je Wewe Unaonaje
Kuhusu hilo?

Chapisha Maoni

 
Top