0
WAKAZI wa eneo la Masasi Mbovu katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara wamefikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani kujibu shitaka linalowakabili la kucheza wakiwa
watupu kwa staili ya vigodoro kwenye sherehe ya ndoa.

Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20), Anna Yohana (25) pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka 17 (Jina linahifadhiwa) walifikishwa mahakamani hapo juzi mbele ya Hakimu Halfani
Ulaya na kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Iddi Athumani.

Athumani alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 30 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika eneo la Masasi Mbovu huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa linalokwenda
kinyume na maadili ya kitanzania.

Alidai kwa kuwa shauri hilo linamshirikisha mtoto aliye chini ya miaka 18, ni vyema Mahakama
ikaahirisha kesi hiyo ili kupisha upelelezi wa kina kuhusu shitaka hilo linalowakabili washtakiwa hao.
Hakimu Ulaya alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka na aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 30 mwaka huu itakapotajwa tena. 

Watuhumiwa hao walio nje kwa dhamana hawakutakiwa kujibu
lolote mahakamani hapo.

Chapisha Maoni

 
Top