0
MGAWANYO wa ruzuku na kikwazo cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vinatarajiwa kugeuka kisu kikali, kitakachotishia muungano wa vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.

Tayari Ukawa imetangaza nia ya kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, na mgombea udiwani, ubunge na urais mmoja katika uchaguzi mkuu ujao, utakaofanyika mwakani.

Mwenyekiti wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, alitoa tamko la mgombea mmoja jana mbele ya waandishi wa habari, ambapo alifafanua kuwa,
mgombea huyo katika kila nafasi kuanzia kitongoji mpaka urais, atateuliwa kwa kufuata vigezo
vitakavyokubaliwa na vyama hivyo.

Alisema uchaguzi huo wa serikali za mitaa, kwao ni nguzo muhimu ya kufikia malengo yao ya kushika dola na hatua hiyo itathibitisha kuwa Ukawa ni ushirikiano thabiti, ulioazimia kuwapa
wananchi njia bora ya ukombozi.
Katika kudhihirisha nia hiyo, Profesa Lipumba alisema Oktoba 26 mwaka huu, wanatarajia kusaini makubaliano ya pamoja ya wanachama wa Ukawa, katika mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

SHERIA
Hata hivyo, tamko hilo la Profesa Lipumba, halikufafanua changamoto iliyotolewa hivi karibuni
na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwamba Ukawa hauwezi kuweka
mgombea mmoja katika mazingira ya sasa ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
Tendwa alitaka vyama hivyo kabla ya kufikia hatua hiyo, vipigie kampeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambao aliuacha
ofisini kwake kabla ya kustaafu, kwa kuwa unaruhusu wao kuungana na kuweka mgombea mmoja.

Kwa mujibu wa Tendwa, kwa sheria ya sasa ya vyama hivyo vinaweza kumuunga mkono mgombea wa chama fulani, lakini haviwezi kuwa
na umoja utakaopewa jina, kisha kusimamisha mgombea mmoja huku kila chama kikibaki na utambulisho wake.
Tendwa ambaye alizungumza na gazeti moja la kila siku, kuhusu utata wa kuweka mgombea mmoja, alisisitiza kwamba Ukawa hawawezi
kuutumia kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu.

Alifafanua kuwa muungano huo wa Ukawa sio wa kisheria, hauwezi kuweka mgombea mmoja wa urais na kumuita mgombea wa Ukawa kwa kuwa
sheria haisemi hivyo.

RUZUKU

Mbali na sheria, Tendwa pia alisema hata utaratibu huo ukianzishwa na vyama hivyo vikapata nguvu ya kisheria kuungana na hivyo kuweka mgombea mmoja, ni lazima upatikane
ufumbuzi kuhusu ruzuku. Kwa mujibu wa Tendwa vyama hivyo vitatakiwa
kujiridhisha ruzuku itakwenda wapi, kama ni katika umoja au chama kupitia mbunge.

Alitoa mfano wa Kenya, ambako Sheria inaruhusu vyama kuungana na kuweka mgombea mmoja, ambako alisema wanachofanya ni asilimia fulani
ya ruzuku kwenda katika umoja na inayobaki kuingia kwenye chama kupitia mbunge. Upungufu uchaguzi
Pamoja na kutangaza nia ya kuweka mgombea mmoja katika uchaguzi wa serikali za mitaa bila kujali mazingira magumu ya kisheria yaliyopo, Profesa Lipumba pia alisema baada ya kupitia
kanuni za uchaguzi huo, wamebaini upungufu mkubwa ambao wanahitaji kupata ufafanuzi wa kina.

Alitaja mambo ambayo alisema yana upungufu kuwa ni idadi ya siku za kuandikisha wapiga kura kutowekwa wazi kwenye kanuni, utata wa fomu za
wagombea na karatasi ya wapiga kura inayohusu wao kutakiwa kujaza nembo ya chama na halmashauri.

Pia alihoji kwanini muda wa mwisho wa kampeni, umewekwa saa 11 jioni wakati kwa Sheria ya Vyama va Siasa inaweka wazi kuwa muda wa mikutano ya siasa ni saa 12 jioni.

Dk Slaa

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema, kwa sasa wanajipangabkuhakikisha Katiba Inayopendekezwa inapingwa
kwa nguvu zote, ambapo alisema watahakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili waikatae katiba
hiyo popote walipo.

“Iwe ni vijiweni kwenye kahawa, mashambani, majumbani au kwingine kokote kule. Tutahakikisha haki za Watanzania zinadaiwa kwa
nguvu zote na kile walichokileta wao (Katiba Inayopendekezwa), kinapingwa kwa nguvu zote,” alisema Slaa.

Hata hivyo,Ukawa watakabiliana na upande mwingine unaotoa elimu ya kuikubali Katiba hiyo, unaoungwa mkono na asasi za kiraia, Chama Cha
Mapinduzi na hata Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mfano, Rais Kikwete alipokuwa ziaranibMwanza hivi karibuni alisema; “Sijui Katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamii kama hii Katiba Inayopendekezwa.
“Hakuna aliyeachwa – wavuvi wamo, wajane wamo, wafanyabiashara ndogo wamo, akinamama lishe wamo, wakulima wamo, wafugaji wamo….kila
mtu yumo.

"Akinamama ndio usiseme kabisa wao wamepata hata asimilia 50 kwa 50 ndani ya Bunge." Aliongeza Rais Kikwete:
“ Hivi Katiba mbaya inakuwa kama
inayopendekezwa na kama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?”

Chapisha Maoni

 
Top