pengine huhitaji kupata
'hug' (kukumbatiwa) ili kujisikia sio
mpweke. Sasa kampuni moja nchini
Japan imetengeneza kiti maalum
ambacho kitakuwa tayari wakati wowote
kumkumbatia na kumliwaza mtumiaji.
Kiti hicho cha "utulivu" kimetengenezwa
kikiwa pamoja na 'mdoli' mkubwa
mwenye sura yenye tabasamu pamoja na
kofia, lakini muhimu zaidi ana mikono
mirefu ambayo inaweza kumkumbatia
mtumiaji.
"Inakufanya ujisikie salama. Kila mtu
anaweza kutumia, lakini zaidi
kimeundwa kwa ajili ya wazee,"
amesema msemaji wa UniCare, kampuni
inayouza kiti hicho.
Karibu robo ya idadi ya wananchi wa
Japan kwa sasa wana umri wa zaidi ya
miaka 65, idadi ambayo inatarajiwa
kuongezeka kwa asilimia 40 katika
miongo kadhaa ijayo.
Kiti hicho kinauzwa kwa yen 46,000 sawa
na dola 419.
Chapisha Maoni