0
MJUMBE wa Bunge Maalumu, John Shibuda, amesema ni heri kuwa msaliti kuliko kuwa mhaini kwa maslahi mapana ya Watanzania.

Shibuda ambaye alipewa nafasi kuzungumza baada ya Katiba Inayopendekezwa kupatikana,
alisema anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lakini amepinga kuwa sehemu ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).

Alisema anajua ataitwa msaliti, jambo alilosema ni vyema kuitwa hivyo kuliko kuwa mhaini wa maslahi ya Watanzania.
Alisema katika mchakato huo, Rais Jakaya Kikwete amewafundisha Watanzania kuwa ni msikivu kiasi cha kusikiliza uongo, huku akijua
kuwa ni uongo lakini akaendelea kusikiliza.

Shibuda alisema utumishi wake ni kwa
Watanzania na kamwe hauwezi kuwa kwa maslahi ya kikundi cha watu.

Kwa mujibu wake, Bunge Maalumu la Katiba, limeepuka watu ambao afya zao za ubongo zina mgogoro, ndio maana wakati wote wanawaza ufedhuli.

Aliwataka wananchi hao kuwa makini na
makatazo ya dini, ambazo zimeasa kuja kwa zama za manabii wa uongo, ambao alisema siasa imegeuka mfereji wa manabii hao.

Chapisha Maoni

 
Top