0
Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.

Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo ambaye kwa mujibu wa jeshi hilo mtu huyo
amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa kuagiza,kuingiza na kuhifadhi mabomu yakivita ya
kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani na kuongeza kuwa
mtandao huo unahusishwa na matukio kadhaa nchini.

Hata hivyo Kamishna Hamdani amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye hata hivyo amekataa kumtaja jina na mazingira ya
ukamataji wake amesema kuwa hauhusiani na imani ya kidini na polisi inamshughulika mtu kisheria kutokana na kosa lake kwa mujibu wa
sheria za nchi na siyo Imani za kidini.

Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yoyote kuhusu mtuhumiwa huyo, jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu akipelekwa nje
ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema bado polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la Zanazibar au ni mtandao wa ugaidi wa
nchi nzima.

Chapisha Maoni

 
Top