0
WATU sita wamekufa maji katika ziwa
Tanganyika na wengine 11 kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi Mariamu Mduwa baada ya mitumbwi
miwili waliyokuwa wakisafiria kutoka
kigoma mjini kwenda katika kijiji cha
Kigalye kilichopo mwambao mwa ziwa
Tanganyika kuzama ziwani.
Tukio hilo limetokea leo saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo kupigwa
wimbi kali na kuzama katika kijiji cha
Kalalangabo wakati bwana harusi huyo
akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani akiwa na ndugu na
jamaa pamoja na wapambe.

Akiongea na Globu ya Jamii katika wodi
namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa
Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo
alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi
sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.

''Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo.

"kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila
namshukuru Mungu kwa kutunusuru na
kifo na yote mimi nimemwachia
Mungu''alisema bibi harusi huyo
Mwathirika mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwabimejaza sana watu na mizigo ndiyo maana
ilizidiwa uzito na kuzama baada ya
kupigwa na wimbi.

''Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima
tupite njia za majini hakuna barabra
kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo
mwambao mwa ziwa Tanganyika
kungekuwa na barabara tungepita
barabrani''alisema Bi Zabibu Issa.
Naye muuguzi wa wodi namba tano
walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa
majeruhi wote waliopo wodini hali zao
zinaendelea vizuri na kwamba mpaka sasa
wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma
Jafari Mohamed akithibitisha hayo alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa, na miili sita kuopolewa pamoja na walionusurika 11.

"Lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili
mingine zaidi ambao bado haijapatikana
kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa
ilikuwa na watu zaidi ya sabini", alisema
na kuongezea kuwa vikosi vya ukoaji kwa
kushirikiana na askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania vinaendelea na
kazi ikiwa ni sambamba na kuchunguza
chanzo cha tukio hilo.

Chapisha Maoni

 
Top