0
KLABU ya Arsenal inakabiliwa na hatari ya ongezeko ya idadi ya majeruhi kufuatia mshambuliaji Danny Welbeck kuumia jana England ikishinda 1-0 dhidi ya Estonia mechi ya kufuzu Euro 2016.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliondoka uwanjani baada ya kuumia enka katika mchezo huo uliofanyika mjini Tallinn na moja kwa moja kuelekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo akiwa na daktari wa England.

Kocha wa Three Lions, Roy Hodgson
ameondoa hofu juu ya maumivu ya Welbeck kwa kusema atakuwa fiti kurejea uwanjani wikiendi. "Sifikiri kama ni majeruhi. Ametonesha enka yake tu kidogo. Madaktari hawana hofu juu ya hilo,"amesema.Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alitua Emirates kwa dau la Pauni Milioni 16 katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia la usajili, na licha ya wasiwasi wa
mashabiki wa Arsenal juu yake, amefunga mabao mazuri manne ikiwemo hat-trick dhidi ya Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa.

Welbeck pia ameendeleza moto wa mabao timu ya taifa ya England tangu aondoke Old Trafford, akifunga mabao mawili dhidi ya Uswisi na lingine dhidi ya San Marino kabla ya jana England ikiendeleza wimbi la ushindi
kwa asilimia 100 kufuzu Euro 2016.

Tayari kocha Arsene Wenger anawakosa
wachezaji 10 Arsenal ambao ni majeruhi, Mesut Ozil, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Olivier Giroud, Mathieu Debuchy, Serge Gnabry, Yannick Sanogo, Theo Walcott na
Laurent Koscielny wakati Calum Chambers atakuwa anatumikia adhabu kweye mechi ijayo. The Gunners watamenyana na Hull City Uwanja wa Emirates Jumamosi katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.

Chapisha Maoni

 
Top