MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure amewajibu kwa vitendo wanaomkandia baada ya kufunga katika ushindi wa 2-0 Manchester
City ikiiangusha Aston Villa Uwanja wa Villa Park.
Yaya Toure alifunga bao hilo dakika ya 82 kabla ya Sergio Aguero kufunga la pili dakika ya 88.
Chelsea, inayoizidi pointi mbili City kileleni mwa Ligi Kuu ya England itacheza na Arsenal kesho Uwanja wa Stamford Bridge.
Kikosi cha Aston Villa kilikuwa: Guzan,
Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley, Westwood, Delph, Richardson/Grealish dk71, Weimann/Benteke dk61 na N'Zogbia/Bacuna dk71.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Milner, Fernandinho/Lampard dk56, Toure, Silva/Navas dk84, Dzeko/Fernando dk64 na Aguero.
Chapisha Maoni