Serikali mkoani kigoma imeyafunga machimbo madogomadogo ya dhahabu katika kata ya Nyamtukuza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, kutokana na kudaiwa kuwa chanzo cha mauaji yawatu watatu yaliyotokea mwishoni mwa wiki kufuatia ugomvi wa kugombea ardhi katika kijiji cha Minyinya.
Akihutubia wananchi katika kijiji cha Minyinya, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amesema, uchunguzi wa awali
umeonesha kuwa chanzo cha mapigano kati ya wakulima na wafugaji ni machimbo ya dhahabu
ya Kanyomvi, Nyamwilonge na Lutela yaliyopo katika kata hiyo ambayo yaliwavutia watanzania kutoka mikoa ya Shinyanga na Geita kuhamia
katika kijiji hicho kwa lengo la kuchimba dhahabu na baadae wakaleta mifugo na kuanza kulima katika mashamba ambayo yanadaiwa kuwa ni ya
wananchi wa kijiji hicho, na kwamba serikali imelazimika kuyafunga ili kuepusha maafa zaidi.
Kwa upande wao, wananchi wa kijiji cha minyinya kata ya nyamtukuza, wamesema kwa muda mrefu
wamekuwa wakipata mateso kutoka kwa jamii ya wafugaji inayoishi katika maeneo wanayolimia kutokana na wao kuyatumia mashamba yao kinyume cha utaratibu, hali ambayo imesababisha
mapigano na watu kuyakimbia maeneo yao , ambapo wameiomba serikali kuwaondoa.
Mapigano kati ya wakulima na wafugaji yalitokea katika kijiji cha minyinya mwishoni mwa wiki na kusababisha watu watatu kuuawa na kuchomwa
moto.
Chapisha Maoni