Chama tawala nchini Sudan kimemteua Rais Omar al-Bashir kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Aprili mwaka ujao. Chama hicho cha National Congress Party
kimesema kuwa jina la Bashir pekee ndilo litakalowasilishwa kwa idhini ya chama hicho katika kongamano litakalofanyika kuanzia Almisi.
Rais Bashir anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kivita
katika jimbo la Darfur ambapo watu 300,000 wameuawa huku wengine milioni mbili wakitoroka kwao tangu waasi walipoanza kupigana na serikali
ya Bashir mwaka 2003.
Amekanusha madai hayo huku Sudan ikikataa kuwa na ushirikiano na mahakama ya ICC. Bashir aliteuliwa kama kiongozi wa chama pamoja
na mgombea mkuu wa chama hicho katika uchaguzi ujao.
Alishinda kuraa 266 kati ya kura 522 na viongozi wa chama wamesema watamwasilisha kwa kongamano la chama ili aweze kuidhinishwa.
Bashir mwenye umri wa miaka 70 alichukua mamlaka kwa njia ya ,mapinduzina kuliwa na utata
ikiwa ataghombea tena katika uchaguzi huo utakaofanyika mwezi Aprili.
Uchaguzi huo utakuwa wa pili tangu mapinduzi yaliyomuingiza mamlakani Bashir mwaka 1989.
Chapisha Maoni