Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la
umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo
Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu
(kushoto),katika mkutano huo Lundenga
alitolea ufafanuzi swala la umri wa
Mrembo huyo kulingana na vilelezo
alivyopewa na mrembo huyo wakati
akijiunga na mashindano hayo
"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya
kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari
hao.
Lundenga aliendelea kusema kuwa
Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiriki, hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto, hilo halina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii
baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
Chapisha Maoni