MANCHESTER City imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na CSKA Moscow ugenini katika mchezo wa Kundi F, Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Sergio Aguero alitangulia kuifungia City bao la kwanza dakika ya 29 akimalizia pasi nzuri ya Edin Dzeko, kabla ya James Milner kuwafungia mabingwa hao wa England bao la pili dakika ya 38.
Seydou Doumbia aliyetokea benchi
akawafungia bao la kwanza wenyeji dakika ya 65 kabla ya Bebras Natcho kusawazisha kwa kwa penalti ya utata dakika ya 86.
Mchezo huo haukuhudhuriwa na mashabiki Uwanja wa Khimki Arena kufuatia adhabu ya CSKA UEFA.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Kolarov, Mangala, Kompany, Zabaleta, Fernando/ Stevan Jovetic dk87, Toure, Milner, Silva/ Frnandinho dk78, Dzeko/Jesus Navas dk72 na Aguero.
CSKA: Akinfeev, Fernandes, V. Berezutski/ Saydou Doumbia dk46/Aleksandrs Cauna dk90, Ignashevich, Shchennikov, A. Berezutski, Natcho, Tosic/Dmitry Efremov dk69, Eremenko, Milanov na Musa.
Chapisha Maoni