BARCELONA imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu wa Camp Nou. Neymar alianza kuifungia Barcelona dakika ya nane kabla ya Lionel Messi kufunga la pili dakika ya 24, Muargentina huyo akitimiza
jumla ya mabao 69 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Messi alifunga bao lingine ambalo lilikataliwa na refa kwa kuwa aliotea dakika ya tatu ya kipindi cha pili, lakini Sandro Ramirez aliyetokea benchi akaifungia Barca bao la tatu dakika za majeruhi.
Bao pekee la Ajax lilifungwa na Anwar El
Ghazi aliyetokea benchi pia. Neymar na
Messi wote walipumzishwa kabla ya dakika ya 66 kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, PSG
imeifunga 1-0 APOEL Nicosia, wakati Kundi H, Shakhtar Donetsk imeichapa 7-0 BATE Borisov na FC Porto imeilaza 2-1 Athletic Bilbao.
Chapisha Maoni