CHELSEA imefanya kile kinachoitwa ‘mauaji’ baada ya kuifumua Maribor mabao 6-0 katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge,
London.
Loic Remy aliifungia bao la kwanza timu ya Jose Moutinho dakika ya 13 kabla ya kuumia na kumpisha mkongwe Didier Drogba aliyekwenda kufunga bao la pili kwa penalti dakika ya 23.John Terry akafunga bao la tatu kwa shuti la mbali dakika ya 30 kabla ya krosi ya Eden Hazard kutumbukizwa nyavuni na beki wa Maribor Mitja Viler katika harakati za kuokoa.
Maribor ilipoteza nafasi ya kupata bao la
kufutia machozi, baada ya mkwaju wa penalti wa Agim Ibraimi kugonga mwamba na Hazard akafunga bao la tano kwa penalti na la sita dakika ya 90.
Katika mchezo mwingine wa Kundi G,
Schalke O4 imeifunga 4-3 na Sporting.
Chapisha Maoni