0
BAYERN Munich imeifumua AS Roma mabao 7-1 katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Olimpico mjini Rome, Italia.
Thomas Muller aliifungia timu ya Pep
Guardiola bao la kwanza dakika ya tisa, kabla ya Mario Gotze kufunga la pili dakika ya 23 na Robert Lewandowski kufunga la tatu baadaye kidogo.

Arjen Robben akafunga la nne akimtungua kipa Morgan De Sanctis kabla ya Thomas Muller kufunga la tano kwa mkwaju wa penalti na Franck Ribery na Xherdan Shaqiri waliotokea benchi wakafunga bao la sita na la
saba. Bao la kufutia machozi la Roma
lilifungwa na Gervinho dakika ya 66. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Manchester City ilitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya CSKA
Moscow.

Chapisha Maoni

 
Top