0
Taarifa kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinaarifu kuwa jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari
wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato
cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.

Habari zinasema kuwa, askari huyo ambaye Septemba 21 mwaka huu alimfungia kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi
huyo na baadaye wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki wakijaribu kutoroka, aliumia kwenye moja ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa
kwenye mahakama ya kijeshi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, pamoja na kukiri kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa
kuweka wazi kama askari huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.

Kamanda Koka aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, jeshi la polisi linafanya uchunguzi juu
ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika, askari huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.

Pamoja na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo, taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi huyo zinadai kuwa, kuna
juhudi za makusudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha mashitaka ya kijeshi dhidi
ya askari huyo. Taarifa zinadai kuwa, polisi wa kituo kikuu cha
polisi mjini Moshi, wanajenga ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo kienyeji.

Chapisha Maoni

 
Top