0
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amelieleza Bunge hilo kuwa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), aliamua kumtukana yeye na Mwenyekiti wa Kamati ya
Uandishi, Andrew Chenge.

“Bwana mmoja Mnyika ameamua kututukana mimi na Chenge…ametuita maharamia mbele ya mkutano wa hadhara huko Mwanza.
“Mimi kwake ni baba yake na kama hawezi kuniheshimu, basi aniheshimu kama mtu mzee katika nchi hii…lakini namsamehe kwa kuwa ni kijana mdogo, huenda ndio anakomaa kisiasa
lakini sisi Watanzania tunatumia lugha yetu kwa staha,” alisema Sitta.

Alifafanua kuwa Mnyika ametoka chuoni juzi juzi na siasa anazoziendesha ni za kivyuo vyuo, ambazo alisema kama ndio zitakuwa siasa za chama hicho, itachukua muda kushika madaraka.
Hata hivyo, alipokuwa akisema ametoka chuo kikuu juzi juzi, wajumbe walipiga kelele wakisema: “Hajamaliza chuo! hajamaliza chuo!”.

Chapisha Maoni

 
Top