wamekubali kukutana na upande wa serikali kujadili malalamiko yao siku tano baada ya maandamano makubwa ya kupigania demokrasia.
Hiyo inafuatia mwaliko kutoka kwa mkuu wa utawala wa Hong Kong CY Leung. Alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda
wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao
waliotishia kuvamia majengo ya serikali iwapoBmkuu huyo hatajiuzulu.
Muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao umemalizika salama.
Bwana Leung amesema atabakia madarakani na kuwaonya waandamanaji kuwa watapata matatizo
iwapo watavamia majengo ya serikali.
Kumekuwa na makabiliano makali katika eneo la majengo ya serikali ambapo waandamanaji wamekuwa wakiendelea kudai uchaguzi wa haki
mwaka 2017.
Chapisha Maoni